Posts

MWANZO WA MAFANIKIO YAK

Katika safari ya mafanikio siku zote mwanzo wake huwa una changamoto, na kama hujapata changamoto mwanzo basi ujue kuna changamoto zipo utakumbana nazo mbeleni. Hii ina maana kuwa mwanzo wa kutafuta mafanikio inahitajika nguvu ya imani kubwa kwa kile ulichopanga kikamilike kwasababu kuna nguvu pinzani inayoleta hofu ya kuanza kukitimiza, hivyo basi kujiamini na kuwekeza nguvu zote inahitajika. Siku zote hasa kuanzisha jambo kama biashara au mradi wowote ule kwanza ondoa ile hofu ya kushindwa na jiambie mwenyewe unaweza ukatimiza kwasababu adui mkubwa pale mwanzo ni hofu. ✓ Hofu ya kushindwa ✓ Hofu ya kuogopa watu watakuonaje ✓ Hofu ya kuanzisha kitu ambacho wengine tiyari wanakifanya na wengine wamefanikiwa Simama wewe kama wewe usiangalie nani anafanya nini labda kwa mazuri tu ambayo yanaleta mafanikio kwa ulichokipanga. Ni mwanzo tu wa kuanza darasa letu la kufanikiwa hasa kiujasiriamali, nikukaribishe sana katika ukurasa huu na uweze kujifunza mengi. Toa maoni...